HALI YA BIASHARA KWA SASA KATIKA SOKO LA MANZESE MKOANI MOROGORO
Hali ya vyakula katika msimu huu wa mfungo
wa ramadhan katika soko la manzese
Manispaa ya Morogoro, imeshuka bei kutokana na wingi wa upatikanaji wa
vyakula hivyo.
Mmoja wa wafanyabiashara wa vyakula katika
soko hilo ISMAILI RASHIDI amesema kuwa, kushuka kwa bei ya vyakula imekuwa ni
hali nzuri iliyopelekea ongezeko la wateja sokoni hapo.
Kwa upande wake mmoja wa wateja wa vyakula Bi. NAWALI MOHAMEDI amesema
kushuka kwa bei ya vyakula, inawasaidia watu wengi kupata mahitaji kwa urahisi
pamoja kuwarahisishia baadhi ya watu walio katika mfungo wa ramadhani.
Hata hivyo BI. NAWALI amewaomba
wananchi walio katika imani ya Kiislamu kutokuogopa kufunga ramadhani kwa
kuhofia kupanda kwa bei ya vyakula kwani vyakula vipo vingi na hupatikana kwa bei
nafuu.
No comments: