JINSI YA KULIMA TANGAWIZI
KILIMO BORA CHA TANGAWIZI
HII NDO MIMEA YA TANGAWIZI
Tangawizi ni moja kati ya aina za mazao ya viungo ambayo sehemu
inayotumika ni tunguu (rhizome). Zao hili kwa lugha ya kigeni linafahamika kama
Zingiber officinale.
UDONGO
NA KUSTAWI
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji mvua kiasi cha milimita 1,200-1,800 na joto la wastani wa nyuzi
joto 20°C-25°C. Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba
na usio-tuamisha maji.
AINA
Mpaka hivi sasa hakuna aina rasmi za tangawizi ambazo
zimeainishwa na kuthibitishwa kuzalishwa nchini Tanzania. Pamoja na hili, kuna
aina tatu za tangawizi ambazo zimezoeleka kuzalishwa na wakulima hapa nchini.
Aina hizo ni Tangawizi nyeupe maarufu kama White Africa au Jamaica,
Cochin
(flint), na Bombay.Tangawizi inayopandwa katika sehemu tambarare
huwa laini zaidi
kuliko inayozalishwa kwenye maeneo ya milima, ambayo huwa ngumu
na kuwa na nyuzi nyingi zaidi.
NAFASI
Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita 23-30 kwa 15-23
na kina cha sentimita 5-10. Unaweza kupanda sehemu yenyemiti au migomba ili
kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia
maji marakwa mara endapo mvua inakosekana hadi kufikia mwezi mmoja kabla ya
kuvuna.
MATUMIZI
Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na
kuchangamsha katika vinywaji kama vile chai, soda, juisi, vilevi na kadha-lika.
Kuna aina mbalimbali za vyakula ambavyo pia hutengenezwa kwa kutumia tangawizi
kama vile mikate,biskuti, keki, nyama zakusaga,acharina kadhalika.Tangawizi pia
hutumika katika viwanda vinavyotengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama
dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi. Hali kadhalika tangawizi
hutumika katika kutengeneza vipodozi vya aina mbalimbali vilekama
poda.
MBEGU NA NAMNA YA KUPANDA
Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu.
Vipande vya tangawizi huhifadhiwa mahali pakavu penye ubaridi ili kuweza
kuchipua.Machipukizi hukatwa urefu wa sen-timita 2.5-5. Baada ya hapo, unaweza
kupanda machipukizi hayo kwenye matuta au shambani kawaida endapo eneo lako ni
tambarare.Baada ya kupanda, tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa
pale kivuli kinapokosekana.
MATAYARISHO
Ondoa takataka zisizohitajika shambani. Wiki 1-2 kabla ya
kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 25-30 kwa hekari moja.
PALIZI
Katika kipindi cha wiki mbili, magugu huanza kuchomoza kwa kuwa
udongo huwa na unyevu kwa wingi. Fanya palizi mara majani yanapojitokeza.
Endelea kung’oa magugu na kuweka shamba katika hali ya usafi hadi wakatiwa kuvuna.
KUPANDA
Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya ardhi, wakati wa masika
hutoa majani juu ya ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu fupi
wakati Cochin ina tunguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya
kijivu na nyekundu. Mmea una urefu wa futimbili na majani yake ni
membamba marefu, ambayo hufa kila mwaka
yakiacha tunguu ardhini likiwa hai. Maua ya mmea huu yana rangi
nyeupe au manjano.
MAGONJWA NA WADUDU
Madoa ya majani: Yanayosababishwa na viini vya magonjwa
viit-
wavyo Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta zingiberi.
Kuoza kwa tunguu: Kunasababishwa na viini viitwavyo Pithium spp.Mizizi
fundo: Inasababishwa na Meloidegyne spp.
UVUNAJI
Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada
ya kupanda, wakati majani yake yanapo-geuka rangi kuwa njano na mashina
kusinyaa.
Tangawizi itakayohifad-hiwa ivunwe mapema kabla haijako-maa
kabisa, na ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi
hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana
kulinganana na huduma ya zao, yanaweza kuwa kiasi
cha tani 20-30 cha tangawizi mbichi huweza kupatikana kwa hekari
moja.
SOKO LA TANGAWIZI
Soko la tangawizi lipo ndani na nje ya nchi, kiasi kikubwa
kinauzwa nchini. Bei yake ni kati sh. 300-1,500/- kwa kilo moja kutegemeana na
msimu.
No comments: