DHANA NA ASILI YA UJASIRIAMALI
SIFA ZA MJASIRIAMALI MJASIRIAMALI
- Ni mtu ambaye yupo tayari kuthubutu
- Ni mtu ambaye ni mbunifu
- Ni mtu jasiri asiye ogopa kufeli au kushindwa
- Ni mtu ambaye kilasiku anatafuta njia mpya za kuzalisha na kuleta upya na mabadiliko
- Ni mtu mvumilivu
- Ni kiongozi
- Ni mshindani asiyekata tamaa
- Ni mtu ambaye anapenda kuwajibika na kazi kwa bidii
- Ni mtu anayetazama maisha ya mbele
- N mtu ambaye anaweza kubadilisha na kutumia nafasi kama fursa.
- Ni mtu ambaye anahitaji na anahamu ya mafanikio
- Ni mtu ambaye anaweza kujitegemea.
Je
wewe unasifa hizo hapo juu? lakini sio lazima uwe nazo zote zilizo
orodheshwa hapo juu, hata sifa chache tu zina kufanya uwe mjasiriamali.
kitu cha kuzingatia ni kwamba baadhi ya sifa mtu huzaliwa nazo na
zingine mtu hujifunza tu, hivyo nawe unaweza jifunza na ukawa
mjasiriamali mkubwa na mwenye mafanikio.
JE UPOTAYARI KUWA MJASIRIAMALI?
kama
unataka kuwa mjasiriamali basi jibu maswali yafuatayo, kama majibu yako
yatakuwa ndio basi wewe ni mjasiriamali lakini kama majibu yako
hayatakuwa ndio basi unaweza kujipanga upya na ukatafuta namana
nyingine ya kueweza kuwa mjasiriamali labda kwa kujifunza dhana za
ujasiriamali.
JIULIZE MASWALI HAYA
1. je umejiandaa kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo?
2. je upo tayari kukumbana na kutatua matatizo na changamoto?
3. je unayafahamu vizuri mazingira unayoishi na je upo tayari kuyatumia na kuanzisha jambo jipya?
4. je upotayari kusubiri kwa muda mrefu matunda ya juhudi zako?
FAIDA ZA UJASIRIAMALI
- kukuza na kuendeleza uchumi katika nchi
- kupunguza umasikini miongoni mwa watu
- ujasiriamali hutusaidia kutumia ipasavyo rasilimali tulizonazo
- matumizi sahihi ya rasilimali watu
- ujasiamali hutupa mwanga katika kufanya na kuanzisha shughli mpya
- ujira binasfsi una nafasi za ajira kwa watu wengi
- hupunguza kiwango cha umasikini miongoni mwa watu
- hupunguza tofauti katika maendeleo baina ya watu, mikoa, nchi n.k
How to Make a Baccarat - FBCASINO
ReplyDeleteIf you're looking for worrione the best guide to playing Baccarat, you've come to the right 바카라 place. kadangpintar Our guide to making it easy to understand the game, tips,