FAHAMU NJIA RAHISI ZA KULIMA MCHICHA
NAMNA YA KULIMA MCHICHA

Mchicha ni mojawapo ya mboga za asili
ambayo hulimwa katika mikoa yote hapa nchini. Mboga hii ina vitamin A, C, na
madini aina ya chokaa na chuma kwa wingi Majani ya mchicha huliwa baada ya
kupikwa au kutengenezwa supu.Mbegu zake zinaweza kusagwa na kupata unga
unaoweza kutumika katika mapishi mbalimbali kama vile kutengeneza ugali, uji,
chapati na maandazi. MAZINGIRA Mchicha unaweza kulimwa karibu katika aina
yeyote ya hali ya hewa na kwenye udongo wa aina yeyote ili mradi usituamishe
maji.
Udongo wenye rutuba nyingi unafaa zaidi
kwa ustawishaji wa zao hili. AINA Kuna aina nyingi za mchicha; zifuatazo ni
aina zinazostawi hapa nchini:- Mchicha Mweupe Aina hii ina majani marefu yenye
rangi ya kijani ya kupauka. Huvunwa kwa kung’oa na huuzwa sana sokoni.Mchicha
Mpana Ni ule ambao ni mnene na una majani mapana na yenye rangi ya kijani
kibichi. Huweza kuvunwa kwa kurudiwarudiwa Mchicha Mwembamba Huu ni mdogomdogo
na unaota shambani kama gugu. Majani yake ni madogo na huchanua mapema.Mchicha
wa Unga Mchicha huu huwa mwekundu unapokuwa mdogo na hukua haraka. Hutoa mbegu
nyingi ambazo zinaweza kusagwa unga, ambao unaweza kutumika kutengeneza vyakula
mbalimbali kama vile, uji na maandazi. Majani yake hupikwa kama mboga au
hutengenezwa supu.
KUTAYARISHA
SHAMBA
Tayarisha shamba mwezi mmoja kabla ya
kupanda. Weka mbolea za asili zilizooza vizuri ili kuongeza rutuba ya udongo.
Mbolea hizi pia hufanya udongo ushikamane vizuri na kuhifadhi unyevu kwa muda
mrefu. Weka kiasi cha ndoo moja yenye ujazo wa lita ishirini katika eneo la
mita mraba mmoja. Changanya vizuri mbolea hii na udongo.
Wiki mbili kabla ya kupanda laininsha
udongo na sawazisha udongo. KUPANDA Kuna niia kuu mbili za kuoanda mchicha,
Kupanda mchicha moja kwa moja shambani na kuotesha miche kwanza kwenye kitalu.
Kupanda Moja kwa Moja Shambani Mbegu hupandwa moja kwa moja kwenye shamba la
kudumu na baadaye mimea hupunguzwa na inayobaki huachwa katika nafasi ya
sentimita 15 hadi 23. Mbegu huweza kupandwa katika sesa au matuta.
Kiasi cha kilo moja hadi mbili za mbegu
kinatosha kuotesha katika eneo la hekta moja. Ili kuepuka mlundikano wa mbegu
sehemu mmoja, changanya mbegu na mchanga kwa kiasi kinacholingana kabla ya
kumwaga shambani. Kisha mwaga na funika kwa kiasi kidogo cha udongo au mbolea
laini za asili. Tandaza nyasi kavu na mwagilia maji.
Endelea kumwagilia kila siku asubuhi na
jioni hadi mbegu zitakapoota. Mbegu huota baada ya siku tatu mpaka tano na
baada ya kuota ondoanyasi. Kuotesha Miche Kwenye Kitalu Kutayarisha Kitalu:
Sehemu itakayooteshwa mbegu inatakiwa iwe laini na yenye rutuba ya kutosha.
Hivyo baada ya kulima lainisha udongo kwa kupigapiga mabonge makubwa.Kisha
tengeneza tuta lenye upana wa mita moja na urefu wowote. Weka mbolea za asili
zilizooza vizuri kiasi cha debe moja au mbili katika kila eneo la mita mraba
moja. Changanya mbolea hii na udongo vizuri, kisha sia mbegu zilizochanganywa
na mchanga kwenye mistari yenye nafasi ya sentimita 10 hadi 15.
Baada ya kusia, funika mbegu kwa kiasi
kidogo cha udongo au mbolea laini za asili. Weka matandazo na mwagilia maji.
Endelea kumwagilia kila siku asubuhi na jioni mpaka mbegu zitakapoota. Baada ya
siku 4 mpaka 6 ondoa matandazo na endelea kumwagilia maji.
Hustawi kwa mda gani?
ReplyDelete