JIFUNZE KILIMO BORA CHA MBAAZI
MMEA WA MBAAZI JINSI YA KUUTUNZA
Hali ya hewa inafaa kwa kilimo kwa
kilimo mbaazi ni nyuzi joto 18 hadi 38sentigredi.mbaazi huwa hazivumialii
barafu .Mbaazi hustawi kwenye mvua kwa mwaka kiasi cha milimita 600 hadi 1000
inagawa aina za muda mfupi hustawi kwenye kiwango kidogo cha mvua milimita
250.hazistawi zaidi kwenye usawa wa bahari
AINA ZA MBAAZI
MBAAZI ZA MUDA MREFU
Huchukua miezi sita mpaka saba shambani mpaka
wakati wa kuvuna.
Zina matawi machache na ni ndefu hvyo hufaa
sana kwa kilimo mseto.haini zinaweza kuvunwa zaidi ya msimu mmoja lakini mazao
yanayopatikana baada ya msimu wa kwanza huwa madogo hivyo inashauriwa aina
zipandwe upya kila mwaka
USTWAI;Aina hizi hustawi vizuri katika ukanda
wa juu na kati wenye mvua za kutosha .
MBAAZI ZA MUDA WA KATI
SIFA ZAKE
Hukomaa ndani ya muda wa miezi minne na nusu
mpaka miezi sita baada ya kupandwa.zina matawi mengi na ni fup kulingana na
mbaazi za muda mrefu.hazikomai zote kwa wakati mmoja humlazimu mzalishaji
kuvuna zaidi ya mara moja ingawa mazao ya kwanza ni mengi kuliko mazao
yanayofata.zinapendwa na kina mama kwa sababu ya mboga kwa jili ya mboga au
enderefu kwa sababu huchanua tena mara zikipata maji
USTAWI;Aina hii ya mbaazi hulimwa katika
ukanda wa kati mita 800 hadi 1100 usawa wa bahari zenye mvua za wastani
MBAAZI ZA MUDA MFUPI
Kundi hili linawakilisha aina bora za mbaazi
za muda mfupi yaani miezi 3 hadi 3 na nusu.
SIFA ZAKE
Aina hii ni fupi ni mita moja hadi moja na
nusu yenye mauwa mekundu inapoanza kuchanua hulimwa katika ukanda wa kati na wa
chini katika uhaba wa mvua kama vile maeneo ya pwani
Aina hii hazichanganywi na mahindi ,inahatari
ya kushambuliwa sana na wadudu hasa ukanda wa kati na wa juu sababu huchanua
wakati wa mvua
Tofauti na aina zote za mbaazi aina hii
haiasiliwi nan a urefu au ufupi wa siku hivyo itachanua wakati wowote mara
baada tu ya kupanda
Haina hii ya mbaazi haina ukinzani wa ugonjwa
wa kunyauka
MATUMIZI YA MBAAZI
Chakula kwa binadamu
Kilimo cha mseto,mbaazi za muda wa kati na
muda mrefu zinaweza kulimwa mseto na mzao mengine ya jamii ya nafaka mfano
mahindi , mtama ,uwere
FAIDA ZA KULIMA MBAAZI NA MAZAO MENGINE
1 Matumizi bora ya ardhi hasa kwa kuwa mbaazi
huongeza ufyonzaji wa hewa ya naitrogen shambani
2 Mzalishaji atapata mazao mawili au zaidi
katika shamba mojana msimu mmoja
3 Kipato cha mzalishaji kitaongezeka kutokana
na mazao mengine
4 Pia mafuno ya mazao ya nafaka kama mahindi
hayapungui kwa kiasi kikubwa kutokana na mchango huo wa mazao
UTAYARISHAJI WA SHAMBA
1 N’goa visiki pamoja na mabaki yote ya mimea
kabla ya uzalishaji
2 Lainisha udongo kwa kupiga halo mbaazi
zinavyoota huwa dhaifu sana na kama shamba halikuandaliwa vizuri magugu huota
mapema kabla ya mbegu za mbaazi
3 Tayarisha matuta au makinga maji kama shamba
lipo kwenye mteremko .
KUANDAA MBEGU
Mbegu bora iliyochaguliwa vizuri na kuhakikiwa
kiwango cha uwotaji iandaliwe
Mbegu ziwekwe dawa za kuzuia kuvu kabla
ya kupanda ili kuzuia magonjwa yatokanayo na mbegu na udongo
MBEGU BORA
Mbegu za mbaazi zimegawanywa kwenye makundi
makuu matatu
1 mbegu ya mda mfupi
2 mbegu ya mda wa kati
3 mbegu ya mda mrefu
UOTESHAJI
Nafasi kutoka mstari hadi mstari hutegemea zao
kuu linalopandwa .kilimo mseto na mahindi hutegemeana pia na aina za mbegu
sentimita 90 mpaka 120 sentimita unashauliwa kutoka mstari hadi msatri 50 sm
kutoka shimo hadi shimo acha mimea miwili kwa shimo
Panda mahindi yanayo komaa mapema ili yavunwe
mapema na kutoa nafasi kwa mbaazi ili kuchanua na kutanuka
Tumia kilo 4 hadi 5 kwa hekari kutegemeana na
ukubwa wa punje
UPANDAJI
Mbaazi za mda mrefu panda kwa mistari kwa
umbali wa sm150 kwa sm100
Mbaazi za muda wa kati panda kwa mstari wa
sm100 kwa 60sentimita
Mbaazi panda kwa umbali wa nafasi sm90kwa
60sentimita
MBOLEA
Mbaazi hustawi vizuri kwenye shamba lenye
mbolea ya kutosha.Hivyo inapendekezwa kwamba kila mzalishaji aweke mbolea ya
samadi ili kuhifadhi arhdi dhidi ya upotevu mkubwa wa mbolea
Jamii ya mikunde hujitengenezea aina ya mbolea
ya naitrogen . hata hivyo tafiti zinaonesha kwamba matumizi ya mbolea za
kupandia kama mabolea ya minjigu ,TSP,OAP,kutaimarisha mizizi na mshina na hivi
kuongeza uzalishaji
PALIZI NA KUPUNGUZA MIMEA
Ni muhimu kuoalilia mapema kuondoa magugu
ambayo hushindana na mimea .palizi ifanyike mara mbili kwa wakati.palizi tatu
inategemea wingi wa majani na unyevu au mvua . mishe ikiwa mingi kwenye shina
husabsbisha mazao kidogo kutokana na mimea kushindania mwanga na virutubisho.
Palizi inaweza kufanyika kwa jembe la mkono au trector kulingana na nafasi
iliyotumika katika kupanda . palizi mbili za mwanzo kati ya siku 60 za mwanzo
ni muhimu kbla ya mbaazi hazijawa na kivuli cha magugu kumea lakini pia kiuwa
gugu kinaweza kutumika kabla ya mbaazi kuota .baada ya mbaazi kuota dhidi ya
magugu ya majani mapana ichanganywe Fluazifopbutyl kudhibiti magugu jamii ya
nyasi,kiuwa gugu kitumike wakati mbaazi zimekua kufikia sentimita 25 hadi 30 .Nimuhimu
kupunguzia miche na kubakiza miwili au kutegemeana na nafasi iliyo tumika
UVUNAJI WA MBAAZI
Mbaazi zikisha komaa na kuanza kukauka zivunwe
mapema kwa kukatwa matawi yenye mbaazi na kukausha zaidi kisha mbaazi
zitenganishe kwa mikono au kwa kupigwa hayo mati taratibu baada ya kukaushwa
sana
No comments: