Header Ads

Breaking News
recent

KIONGOZI NI NANI? NA SIFA KUU 10 ZA KIONGOZI.

Kiongozi ni mtu ambaye huongoza kikundi cha watu[1]. Mara nyingi kiongozi hupewa heshima ya juu katika jamii, kikundi cha watu au katika familia ambapo huheshimiwa na watu wote katika eneo husika analolisimamia kiongozi kwa ajili ya kuwaongoza watu.

MHE. SAMIA SULUHU HASSAN
MHE. SAMIA SULUHU HASSAN.Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
SIFA KUU 10 ZA KIONGOZI BORA.
1.uwazi.
  Uwazi ni sifa muhimu inayomfanya mtu kuwa kiongozi Bora.kiongozi Bora lazima awe wazi katika utendaji kazi wake iwapo Kuna siri za kazi, ila namna ya utendaji kazi wako hautakiwi uwe Siri au usioeleweka kwa wale unaowaongoza. 
2.MAONO.
    Maono ni picha inayojengeka katika fikra ya matokeo ya jambo ambalo linapangwa kutekelezwa. Kama wewe ni kiongozi asiyejua kuona picha ya badae ya mafanikio na malengo yake hutaweza kuongoza taasisi,kampuni nk.lazima kiongozi ujifunze kua na maono katika kila Jambo unalolifanya ili ufanikiwe.
3.UADILIFU.
   Ili uwe kiongozi Bora huna budi kuwa mwadilifu.heshimu kazi,tunza muda na tunza fedha pia tumia nafasi yako kwa njia ambayo si ya kibadhirifu.
4. UJASIRI.
    Huwezi kuwa kiongozi Bora Kama hutakuwa na ujasiri katika Mambo mbalimbali. Unatakiwa kuwa jasiri kwenye maamuzi unayoyafanya katika eneo unayoongoza, Kama vile kubadili mfumo wa uwekezaji kwenye kampuni nk.
5.SUBIRA.
    Kuwa kiongozi mkomavu kifikra lazima uwe subira na uvumilivu wa kufanya maamuzi kwa haraka pasipo kufikiri vizuri. Kwa mfano  Wakati mwingne taasisi au kampuni inaweza ikawa inapitia wakati mgumu pasipo subira unaweza ukafanya maamuzi yatakayoathiri kabisa.
6.MBUNIFU.
   Kufanikiwa kwa kiongozi kunahitaji ubunifu wa hali ya juu kila mara ili kujitofautisha na wengine waliokwisha kupita.hivyo Basi ili uwe kiongozi Bora lazima ujitahidi kuwa mbunifu.
7.UWAJIBIKAJI
   Ukitaka kuwa kiongozi Bora huwezi kujitenga na uwajibikaji. Lazima uwajibike katika kutimiza majukumu yako yote. Swali la kujiuliza ni kwamba unawezaje kumhimiza mtu kutimiza wajibu wake Kama wewe Kama kiongozi umeshindwa kutimiza wajibu wako?. Nasisitiza kwa kusema kuwa ili uitwe kiongoz Bora na sio bora kiongozi wajibika kwenye nafasi yako kwanza na wale unaowaongoza watawajibika pia.
8.KUJITUMA.
   Kujituma ni Jambo muhimu sana kwa kiongozi Kiongozi Bora hahitaji usimamizi mkali ili atimize majukumu yake. Hivyo Basi jifunze kujituma bila kusukumwa na mtu fanya bidii ya kujituma katika uongozi wako.
9.MAWASILIANO.
    Mawasiliano ni Jambo muhimu sana linalojenga utawala bora. Katika uongozi wowote ikitoke hakuna mfumo mzuri wa mawasiliano kunatokea migongano isiyo na sababu. Hakikisha unakua na mfumo mzuri wa mawasiliano na watu unaowaongoza na inakuwa na utaratibu mzuri wa utoaji wa tarifa.
10.NIDHAMU.
     Kuna Mambo ambayo huwezi kufanya ukiwa Kama kiongozi hata Kama unavutiwa navyo. Siku zote epuka tabia zisizo endana na kiongozi Bora, Kama vile ulevi, umbea, anasa, uvivu, kuongea ovyo,starehe nk. Fanya watu unaowaongoza wajue wewe ni kiongozi unaejitambua na kuwa na nidhamu ya kiutawala.

By ZUHURA AMANI MTERA JOURNALIST. nitafute kwenye mitandao ya kijamii Facebook zuhura Amani, WhatsApp 0677494573, Instagram official zuu7, Twitter zuhura Amani, email zuhuraamani24@gmail.com.
YOUR WELCOME TO MY BLOG.

No comments:

Powered by Blogger.