UFUGAJI WA SAMAKI KIBIASHARA
MBINU MUHIMU WAKATI WA
UANZISHAJI UFUGAJI WA SAMAKI
• Mfugaji anatakiwa awe na shauku na dhamira ya
kweli ya ufugaji.
• Kufanya tathmini ya rasilimali alizonazo kwa ajili
ya mradi wa ufugaji wa samaki.
• Chanzo endelevu cha mtaji kwa ajili ya mradi.
• Hulka ya uvumilivu na kuthubutu.
• Tathmini ya soko la bidhaa za samaki.
• kujipatia maarifa ya msingi ya ufugaji wa samaki
SIFA ZA ENEO LA KUFUGIA
SAMAKI
• Eneo la kufugia samaki linatakiwa liwe na maji
ya kutosha kwa mwaka mzima.
• Eneo la kufugia samaki linatakiwa liwe na
udongo unaoweza kutuamisha maji.
• Eneo zuri la kufugia samaki ni kuwa eneo lisiwe
na historia ya mafuriko, kwa kuwa mafuriko
yakitokea samaki waliokuwa bwawani
wataondoka na maji na bwawa litafunikwa na
udongo.
• Eneo zuri la kufugia samaki ni lile linalofikika
kwa urahisi.
• Eneo la kufugia samaki pia linatakiwa kuwa ni
eneo lenye amani na utulivu na watu wenye
kuelewana.
• Kuwa na soko la bidhaa.
• kuwa na umiliki wa ardhi wa uhakika.
UTENGENEZAJI WA BWAWA LA SAMAKI.
Zipo namna mbalimbali za utengenezaji wa
bwawa la samaki, kulingana na aina ya bwawa
lenyewe, Hali ya uchumi, wingi wa samaki
watakaofugwa pamoja na aina ya samaki
watakaofugwa.
Zifuatazo ni Aina za mabwawa ya kufugia
samaki.
1.Bwawa la kuchimba udongo bila kujengea
"Earthen Pond.
2. Bwawa la kuchimba udongo na kujengea kwa
Matofali, Simenti na Zege.
UANDAAJI NA UPANDIKIZAJI WA
VIFARANGA AU MBEGU ZA SAMAKI
KATIKA BWAWA LAKO.
Kabla ya kuvisafirisha vifaranga kutoka kwenye
bwawa wanaloishi ni vema vikatolewa na kuwekwa
kwenye vibwawa vidogo vidogo kwa muda wa kati
ya saa 24 hadi 72 (kutegemeana na umbali wa
safari) bila chakula. (???)
• Wakati wa kupandikiza mfugaji anatakiwa akifika
asivimwage vifaranga kwenye bwawa bali
anatakiwa kuyaruhusu maji yaliyobeba vifaranga
yabadilishane ujoto na maji yatakayopokea
vifaranga. Hapa mfugaji anatakiwa kuliweka
kontena au chombo alichobebea vifaranga kielee
kwenye maji anayotaka kufugia kwa muda wa
dakika kati ya 30 hadi 35, baada ya hapo chombo
kilicho na vifaranga kifunguliwe na kiinamishwe
ili maji hayo yaweze kukutana na yale
yaliyoandaliwa kwa ajili ya kufugia na hapo
ataruhusu vifaranga kuingia wenyewe kwenye
bwawa husika.
• Iwapo utafika na kuvimwaga vifaranga kwenye
bwawa jipya bila kufuata utaratibu huo wa
kitaalamu basi tofauti ya ujoto wa maji kati ya
chombo kilichosafirishiwa vifaranga na bwawa
unaweza kusababisha vifaranga wote kufa kwa
muda mfupi, kitaalamu wanasema kuwa vifo vya
vifaranga hivyo vinasababishwa na mshituko wa
joto.
• Jambo lingine la kuzingatia ni kuwa uandaaji
na usafirishaji wa vifaranga ni vizuri
ukafanywa muda ambao hali ya hewa inakuwa
na ubaridi. Muda unaopendekezwa zaidi na
wataalamu ni asubuhi au jioni kwa sababu
muda huo samaki wanakuwa na uwezo wa
kuhimili misukosuko ya safari tofauti na hali
ya hewa inapokuwa ya joto.
Hi
Kimsingi hakuna tofauti kubwa wala athari
kubwa sana za ufugaji wa samaki wakati wa
kiangazi ukilinganisha na wakati wa masika,
tofauti zilizopo ni ndogo ndogo ambazo
kitaalamu hazina madhara makubwa kwa
mfugaji.
ulaji wa chakula wa samaki na ukuaji wao
uchafuzi wa maji yanayoingia kwenye
mabwawa ya kufugia
ULISHAJI NA UTUNZAJI WA
SAMAKI BWAWANI.
• Samaki wapewe chakula angalau mara 2 kwa siku
(saa 3-4 asubuhi na 9-10 jioni) /hewa ya kutosha .
• Kuwapa vyakula tofauti kutegemeana na silka ya
aina ya samaki unaowafuga.
• Kuna samaki wanaofaidika na vyakula vya nyama
nyama kama vile kambale na sangara (hawa hawali
pumba) na kuna samaki wengine kama sato
wanakula vyakula mchanganyiko wa nyama na
mboga mboga na wapo wengine wanaokula vyakula
vyenye asili ya mimea tu “carps”.
TABIA ZA ULAJI WA SAMAKI
1) Samaki wanaokula nyama, (sangara na
kambale).
2) Samaki wanaokula mimea ‘carps’.
3) Samaki wanaokula vyakula mchanganyiko
(nyama na mimea) kama perege, sato na
mwatiko (samaki wa maji chumvi).
MUONGOZO WA MAHITAJI YA
VIINILISHE VYA SAMAKI
Wanga 20-25%
Mafuta 10-15%
Vitamin 1-2%
Madini 1-2%
Protini 18-45%
NB; Maji – hapa ifahamike kuwa wakati
tunazunguzia viwango vya maji vinavyohitajika
kwa wanyama wengine wafugwao, hitaji la maji
kwa samaki ni ubora wa maji anayofugiwa na sio
wingi wake.
TARATIBU ZA ULISHAJI WA
SAMAKI.
Umri (Wiki) Uzito (gm) Kiasi cha
chakula kwa
siku(gm)/samaki
1-2 5-20 1gm
2-3 20-50 2gm
3-5 50-110 3gm
5-7 110-200 4gm
7 mpaka
mavuno
200gm na zaidi 5gm
MASOKO YA SAMAKI
Soko la awali, hili ni soko la moja kwa moja
kutoka kwa muuzaji ambaye ni mfugaji kwenda
kwa mlaji,
Soko la kati, katika soko hili kwa kawaida
kunakuwa na mtu wa kati ambaye ananunua
samaki kwa mfugaji kwa lengo la kwenda
kuwauzia walaji.
Soko la kimataifa, hili ni soko linalofanyika nje
ya nchi (baina ya nchi moja na nchi nyingine).
Kwa ushauri zaidi wasiliana NAMI kupitia namba ya Whatsapp 0677494573 au kwa email zuhuraamani24@gmail.com..
No comments: