FAHAMU KILIMO CHA TANGAWIZI
1. UTANGULIZI:
Jina la kitaalamu ni Zingiber officinale
Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo
sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome)
ambalo huonekana kama mizizi ya mmea.
Asili ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya
bara la Asia na hasa katika nchi za India
na China. Zao hili linazalishwa kwa wingi
kutoka katika nchi ya Jamaica. Hapa nchini
zao hili hulimwa katika mikoa ya Kigoma,
Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na
Kilimanjaro.
Tangawizi hutumika kama kiungo katika
kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha
katika vinywaji (kama soda, juisi, vilevi
n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate,
biskuti, keki, nyama za kusaga, achari n.k.
Hutumika pia katika viwanda
vinavyotengeneza madawa ya tiba
mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi,
tumbo na muwasho wa ngozi n.k. pia
hutumika katika vipodozi kama poda n.k).
2.AINA ZA TANGAWIZI
Hakuna uthibitisho wa aina za tangawizi
ambazo hulimwa hapa nchini ila kuna dalili
ya kuwa na aina za White Africa (Jamaica)
na Cochin (flint); hii huwa na tunguu
ngumu zenye nyuzi.
3.TABIA YA MMEA
Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya
ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu
ya ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya
kahawia na tunguu fupi wakati Cochin ina
tunguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo
kati ya kijivu na nyekundu. Mmea una
urefu wa futi mbili na majani yake ni
membamba marefu ambayo hufa kila
mwaka yakiacha tunguu ardhini likiwa hai.
Maua ya mmea huu yana rangi nyeupe au
manjano.
4. HALI YA HEWA NA UDONGO
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali
ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi
mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji
mvua kiasi cha mm.1,200-1,800 na joto la
wastani wa nyuzi za sentigredi 20-25.
Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye
rutuba na usiotuamisha maji.
5.UPANDAJI
Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia
vipande vya tunguu vyenye kichipukizi
kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa
katika urefu wa sm.2.5-5. Wakati
mwingine, vichipukizi vinavyopatikana
katika kumenya tangawizi huweza
kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda.
Kiasi cha kilo 840-1700 cha vipande vya
tunguu huweza kutumika kwa kupanda
katika hekta moja.
Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya
sentimita.23-30 kwa 15-23 na kina cha
sentimita.5-10 na mara nyingi hupandwa
katika matuta. Baadhi ya mazao huweza
kupandwa katika shamba la tangawizi ili
kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima
kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji
endapo mvua inakosekana.
iki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya
samadi au mboji kiasi cha tani 25-30 kwa
hekta na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK
kwa uwiano wa kilo 36:36:80. Tandaza
nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu
hasa pale kivuli kinapokosekana.
Palizi hufanywa mara magugu yanapoota,
dawa ya kuua magugu, kama simazine
hutumika.
7.0 Magonjwa na wadudu:
• Madoa ya majani yanayosababishwa na
viini vya magonjwa viitwavyo
Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta
zingiberi.
• Kuoza kwa tunguu; kunasababishwa na
viini viitwavyo Pithium spp
• Mizizi fundo; inasababishwa na
Meloidegyne spp.
8.UVUNAJI
Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna
kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda,
wakati majani yake yanapogeuka rangi
kuwa njano na mashina kusinyaa.
Tangawizi inayohitajika kwa kuhifadhi
kwenye kemikali (preserved ginger in
brine) huvunwa kabla haijakomaa kabisa,
wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi
na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa
kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana
kulinganana na huduma ya zao, mavuno
yanaweza kuwa kiasi cha tani 20-30 cha
tangawizi mbichi huweza kupatikana.
9.USINDIKAJI
Tangawizi ikisindikwa utapata unga,
mafuta maalum (essential oils) n.k.
Tangawizi iliyovunwa huweza kumenywa,
kukatwa na kukaushwa juani au mara
nyingine huchovywa katika maji
yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa
au hukamuliwa mafuta.
Pia tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa
kwenye chupa zikiwa zimechanganywa na
sukari na/au chumvi. Hata hivyo tangawizi
ina Kiasi cha mafuta cha
16.0-18.0%.
10. SOKO LA TANGAWIZI
Soko la tangawizi lipo ndani na nje ya nchi,
kiasi kikubwa kinauzwa nchini. Bei yake ni
kati sh. 50000- 60000/-
KWA HABARI ZAIDI WASILIANA NAMI KWA email-zuhuraamani24@gmail.com. WhatsApp 0677494573.
No comments: