MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ZASABABISHA MFUMKO WA BEI ZA MATUNDA MKOANI MOROGORO.
21
APRIL 2018 MOROGORO BIASHARA
Mwenyekiti wa soko la Mawenzi Manispaa ya
Morogoro Ramadhani Mohamedi,
ametoa ufafanuzi juu ya hali ya Biashara ya Matunda hasa katika kipindi hiki cha Mvua
zinazoendelea kunyesha mkoani hapa.
Mohamedi
amesema kuwa, kuna baadhi ya bidhaa ambazo zimepanda bei hususani
vitunguu na Nyanya kutokana na hali ngumu ya usafirishaji wa bidhaa hizo kutoka mashambani hadi sokoni hali
inayosababisha bidhaa hizo kuoza.
“Matunda
niseme pia msimu bado haujachanganya lakini mvua nazo zinachangia kwasababu usafirishaji
wa matunda kutoka mashambani unategemea magari na barabara kwa sasa ivi
barabara zimekuwa sio nzuri na matunda yakifika sokoni yakiwa yameharibika
inasababisha bei kuuzwa kubwa”
Aidha Mfanyabiashara wa matunda katika soko
hilo Imani mhawi, amesema kuwa msimu huu
wa mvua zinazoendelea kunyesha imesababisha bei za matunda kupanda kwa kasi,
pia wamekuwa na changamoto ya wanunuzi wengi
kushindwa kufika sokoni kwa wakati.
“Changamoto
tunazokutana nazo ni usafirishaji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na
matunda kutoka kule shambani mpaka yafike sokoni yanakuwa yameharibika”
No comments: