NJIA TATU (3) PEKEE ZA KUKUZA BIASHARA
1. Ongeza Idadi Ya Wateja.
Nafikiria unafahamu kuwa wateja ndio
wanaokuingizia pesa katika biashara yako.Na kila ukiwa na wateja wengi
ndivyo kipato kinavyozidi.Na kila wanavopungua ndivyo kipato kinapungua na
hatimae kuuwa biashara yako.
Je Wateja
Wako Utawapata Wapi?
Wateja hawapatikani isipokuwa wewe
(au hata watu wengine) kutangaza kwa watu kuwa una biashara fulani yenye kutoa
bidhaa au huduma fulani.Na njia kuu ya kupata wateja ni kutangaza.Na matangazo
unaweza kufanya kwa njia mbili.
1.
BURE –
Kuwa na duka au ofisi sehemu iliyo mbele za nyuso za watu, kuongea na watu ana
kwa ana, kutumia mitandao ya kijamii n.k
2.
Kulipia matangazo –
Hii itakusaidia kuwafikia maelfu ya watu kwa mpigo kitu ambacho kitakusaidia
kuongeza idadi ya wateja wapya mara moja.
2. Ongeza Idadi Ya Mauzo Ya Kila
Mteja.
Kama kila mteja anakuingizia wastani
wa shilingi elfu kumi kwa kila manunuzi, inabidi ujitahidi kumshawishi mteja
huyo kununua bidhaa za ziada zitakazokufanya uongeza mapato kwa kila manunuzi.Swala
la kujiuliza ni bidhaa gani ya ziada unayoweza kuwauzia wateja
wako juu ya kile kitu wanachonunua kila siku.
Mfano biashara ya hoteli umepewa oda ya burger, wanakuuliza “je utapenda
tukuwekee na chipsi katika hiyo burger?” ukisema ndio wanakuuliza tena
“utapenda tukuwekee na kinywaji gani?”Wewe na yako ilikuwa ni burger pekee yake
lakini umejikuta unanunua na chipsi na soda.
3. Ongeza Idadi Ya Mauzo
Endelevu.
Jambo la tatu la muhimu kufanya ni
kuhakikisha wateja wako wanarudi kwako mara kwa mara kununua bidhaa au huduma
unayotoa.Unaweza kufanya hivi kwa:
1.
Kuuza bidhaa au huduma inayopendwa na wateja wako
2.
Kuwasiliana na wateja wako mara kwa mara kuwajulisha kuhusu OFA
au bidhaa au huduma mpya ambazo umezileta kwa wakati huo.
No comments: