Namna ya kulisha kuku Ili wasipatwe na magonjwa
Ili uweze kuepusha magonjwa kwa kuku zingatia
mambo haya yafuatayo:
Safisha
vyombo vya kulishia na kunyweshea kila siku. Osha, sugua vizuri, kisha suuza
kuondoa utando unaobeba bakteria.
Kuku
wanahitaji wapewe chakula cha kutosha na chenye virutubisho vyote. Unaweza
kuwaongezea majani, makombo, nafaka, mchanga laini, au maganda ya mayai.
Wapatie
kuku maji safi muda wote. Wafugaji wengi wameripoti kuwa na matokeo mazuri
baada ya kuchanganya dawa ya kuua vimelea kwenye maji ya kunywa.
Nunua
chakula kwa wauzaji wazuri na wanaoaminika ili kuepuka minyoo na sumu
hatarishi. Usiwape kuku chakula chochote kinachoonekana kuoza au kunuka uvundo.
Hifadhi
chakula cha kuku katika sehemu kavu isiyo na joto na isiwe kwa zaidi ya miezi
mitatu ili kuepuka kuharibiwa na fangasi.
Kwa taarifa zaidi ntafte kwa namba watsap 0719257061 au kupitia email yangu
zuhuraamani24@gmail.com
No comments: