Header Ads

Breaking News
recent

SOMA JINSI YA KUFANYA BIASHARA KWA WELEDI SANA


UJASIRIAMALI NI MUHIMU KWA MAENDELEO ENDELEVU TANZANIA.
Nini maana ya Ujasiriamali na Mjasiriamali?
    Mjasirimali ni yule mtu anayegundua au anayeboreasha wazo la biashara.
     Ujasiriamali ni kile kitendo cha kubuni au kuboresha wazo la biashara na kulifanyia kazi ya aidha kuuza bidhaa au kutoa huduma. Kwenye hili, mtu anakua na wazo ambalo anataka kulifanyia kazi ili apate faida baada ya kulitekeleza.
                  SIFA ZA MJASIRIAMALI
kuna sifa za jumla ambazo wajasiriamali wengi huwa nazo. Sifa hizo ni kama zifuatazo:
i.Ubunifu
Hii ni moja ya sifa ambazo mjasiriamali ni lazima awe nazo. Mbunifu ni yule mtu mwenye uwezo wa kuja na mawazo ya kuwa na huduma au biashara mpya inayohitajika sokoni. Kuwa mbunifu haimaanishi kuwa mtu anakuja na mawazo mapya kila mara, ila inaweza kuwa ni uwezo wa kuja na mbinu au njia mpya za kutengeneza, kuuza au kutangaza bidhaaa au huduma ambayo tayari ipo.
ii.Kuwa mtu wa kushikilia na kuhangaikia kukamilisha malengo unayojiwekea
Mtu mwenye malengo ni yule mtu ambae anashikilia nakukazania malengo ambayo amejiwekea. hii ni sifa nyingine ya mjasiriamali mzuri, kwa maana kama hautajiwekea na kushikilia malengo yako binafsi ni rahisi sana kuyumbishwa na matatizo madogo madogo yanayoweza ikumba biashara yako. Lakini ukiwa na malengo thabiti, nirahisi kuwa na jibu kwenye kila tatizo unalopata.
iii. Kujiamini
Mara nyingi kujiamini huja baada ya kuwa na malengo thabiti ukishakuwa na malengo thabiti kinachofuata ni kuamini mipango yako italipa. Kujiamini ni muhimu kwa sababu kuna kupa nguvu ya kukabiliana na vikwazo vinavyoweza kuiikumba biashara yako.
iv. Kufanyakazi kwa Juhudi
Cha mwisho, mjasiriamali ni lazima afanye kazi kwa bidii. Kufanyakazi kwa bidii haimaanishi mjasiriamali afanye kazi zote yeye mwenyewe, inamaanisha awe tayari kupunguza mambo mengine na kuwekeza muda mwingi kwenye biashara yake. Mara nyingi, kuwa mjasiriamali kunamaanisha wewe ndio bosi wa biashara yako, hivyo nilazima uwe na nidhamu ya kujisimamia na kusimamia watu wengine wanaokusaidia katika biashara yako.

Mteja ni nani?
Mteja ni mtu au tasisi yoyote ambaye una uhusiano naye katika biashara. Si lazima mteja awe ni yule anayenunua bidhaa au huduma kutoka katika biashara yako leo.
Hata yule mtu anayekuja kuulizia au kutembelea biashara yako ni mteja vilevile.
Vidokezo vya kujenga uhusiano mwema na wateja.
Kila mara msalimie mteja na kisha muulize “ Naweza kukusaidia”?
Kwanza jifunze kuwa msikilizaji mzuri. Sikiliza na kuelewa.
Kama hujaelewa, uliza ili kukidhi haja ya mteja.
Kuwa mkarimu kwa wateja wote. Wahudumie kwa tabasamu. Watimizie wanachotaka kwa utaratibu ulio wazi.
Wahudumie wateja kwa makini.
Ruhusu wateja wazijaribu bidhaa zako (inapobidi).
Kubali malalamiko na ujibu kwa uangalifu.
Zungumza kidogo, onyesha zaidi.
Uza manufaa, siyo bidhaa pekee.
Kila mara jaribu kuwa na subira, kwasababu wateja wengine ni wazito kuamua.
Mambo Yasiyofaa
Usibishane na mteja
Usimchanganye mteja kwa maelezo mengi mno.
Usimuuzie mteja zaidi ya kile anachoweza kutumia
Usikate tamaa mteja anaposema kwamba bei ni kubwa mno. Badala yake mweleze manufaa atakayopata
Usimlazimishe mteja kununua, bali mshawishi.
Usimkatize mteja anapozungumza, yeye ndiye mfalme.
Usinywe, usivute, wala usile unapokuwa unauza, hivi ni vitendo vinavyoweza kumkera mteja.
Mambo ambayo huweza kuharibu uhusiano na mteja
Uso wenye hasira
Uso unaoonyeha kusononeka au kuchoka.
Kutojali mteja anapokuja
Kutoa huduma kwa upendeleo
Kuonyesha kutokuwa na ujuzi katika utoaji huduma
Kutoa huduma pole pole sana
Lugha isiyofaa
Kukejeli wateja
Kumdai mteja kitu kilicho nje ya utaratibu ndipo huduma itolewe
Kutotekeleza ahadi
Kupokea zawadi kutoka kwa wateja (zenye nia ya kutoa upendeleo)
Kujenga mahusiano ya kimapenzi na wateja
Kutowatimizia wateja mahitaji yao
Kupiga soga wakati wateja wanasubiri
Kutoa huduma huku umelewa.
Kushindwa kutoa faraja kwa wateja wakati inapobidi wasubiri huduma


Kwa fundisho zaidi tembelea ukrasa wangu wa facebook (zuhura Amani)  na tweter (Zuhura Aman) watsap (0719257061) email. zuhuraamani24@gmail.com.

No comments:

Powered by Blogger.