USIMAMIZI WA RUTUBA YA UDONGO KATIKA KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO
RUTUBA YA UDONGO
Rutuba ya udongo ni nini?
Rutuba ya udongo inafafanuliwa kwa uwezo wake wa kutoa virutubisho vyote muhimu kwa kiasi kinachotosheleza na katika urari sahihi kwa ajili ya ukuaji wa mimea, bila ya kutegemea matumizi ya moja kwa moja ya virutubisho, wakati vipengele vingine vya ukuaji kama vile mwanga, nyuzi joto na maji viko katika hali inayofaa. Uwezo huu hautegemei kwenye wingi wa virutubisho kwenye udongo peke yake, lakini pia kwenye ufanisi wa kubadilisha virutubisho ndani ya duara la virutubisho shambani. Katika kubadilisha virutubisho, viumbe vya udongo vina jukumu muhimu. Huvunja vunja majani na sehemu nyingine zinazotokana na mabaki ya mazao shambani, mbolea ya kijani na matandazo na kuchangia katika kuongeza mabaki ya viumbe hai, ikiwemo na mboji, hazina ya virutubisho muhimu zaidi kwenye udongo. Viumbe hawa pia hutekeleza jukumu muhimu la kuhamisha mabaki ya viumbe hai kwenye udongo hadi hatua ya kuwa mfumo wa madini, ambayo yanaweza sasa kutumika na mimea. Viumbe vya udongo pia hulinda mimea dhidi ya magonjwa na kufanya udongo umeng’enyeke. Ni rahisi kufanya kazi kwenye udongo wenye rutuba, hunyonya maji ya mvua vyema na ni thabiti dhidi ya kujaa tope na mmomonyoko. Huchuja maji ya mvua na kutupatia maji safi ya kunywa. Huzimua (huzuia) tindikali, ambalo hupita kwenye hewa chafu na kutua juu ya udongo, na kuozesha kemikali zinazochafua mazingira kama vile viuatilifu haraka. Na mwisho japo pia ni muhimu, udongo wenye rutuba ni hazina ya ufanisi ya virutubisho na hewa ya kaboni (CO2 ). Kwa njia hii udongo wenye rutuba huzuia mlundikano wa virutubisho kwenye mito, maziwa na bahari na kuchangia katika kupunguza kupanda kwa joto duniani. Katika mazingira ya kilimo cha kibiolojia, rutuba ya udongo kimsingi ni matokeo ya michakato ya kibiolojia na sio virutubisho vya kikemikali. Udongo wenye rutuba uko katika mbadilishano ulio hai na mimea, hujiumba upya na una uwezo wa kujifufua. Sifa za kibiolojia zinaweza kuonekana katika shughuli za ubadilishaji zinazofanyika kwenye udongo, katika uwepo na dalili zinazoonekana za viumbe ndani yake. Jamii ya vijidudu iko thabiti na hufanya kazi katika muda stahiki. Katika mahusiano ya kiekolojia yanayojidhibiti yenyewe, wanyama, mimea na vijidudu wote hufanya kazi kwa manufaa ya wote. Ni jukumu la wakulima kuelewa ekolojia ya udongo hadi kufikia mahali ambapo wanaweza kujenga au kurudishia hali ya uwiano thabiti kwenye udongo. Kama udongo utakuwa hauleti mavuno mazuri mara kwa mara, wakulima wanapaswa kuchunguza sababu ya kufanya hivyo.Sifa za udongo wenye rutuba
Udongo wenye rutuba:
a) una virutubisho vingi muhimu kwa ajili ya lishe ya msingi ya mmea (ikiwemo naitrojeni, fosfora, potasiam, kalsiam, magnesia na salfa kwa kupima virutubisho ndani ya udongo utawasiliana na mimi kwa namba za simu mwishonib) una virutubisho vya kutosha vinavyohitajika kwa kiwango kidogo sana na mmea (ikiwemo boroni, kopa, chuma, zinki, manganizi, klorini na molibdenam);
c) una kiasi stahiki cha mabaki ya viumbe hai kwenye udongo;
d) una kipimo cha pH katika kiwango kinachofaa kwa ajili ya uzalishaji wa mazao (kati ya 6.0 na 6.8 pia kwa kupima pH wasiliana na mimi)
e) una muundo unaomeng’enyuka;
f) uko hai kibiolojia;
g) una uwezo mzuri wa kuhodhi maji na kutoa virutubisho
Kiasi stahiki cha virutubisho vya mmea
UPIMAJI WA VIRUBISHO VYA UDONGO |
Vitu vinavyowezesha mizizi kufyonza virutubisho kwenye Udongo
a) Kwanza, udongo lazima uwe na unyevu wa kutosha kuruhusu mizizi ichukue na kusafirisha virutubisho. Wakati mwingine kuipatia mimea maji kutaondoa dalili za upungufu wa virutubisho.b) Pili, kipimo cha kupima uasidi cha pH ya udongo lazima kiwe katika kiwango fulani ili virutubisho viweze kuachiwa kutoka kwenye punje za udongo.
c) Tatu, nyuzi joto ya udongo lazima iwe katika kiwango fulani ili unyonyaji wa virutubisho uweze kutokea.
d) Nne, virutubisho lazima viwepo karibu na eneo la mizizi ili mizizi iweze kuvifi kia.
Kiwango cha nyuzi joto, pH na unyevu ni tofauti kwa aina tofauti za mimea. Kwa hiyo kihalisia virutubisho vinaweza kuwepo kwenye udongo, lakini visiweze kunyonywa na mimea. Ujuzi wa pH ya udongo, umbile asili na historia unaweza kuwa wa manufaa sana kwa kutabiri ni virutubisho gani vinaweza kuwa pungufu. Kwa upande mwingine, virutubisho vikizidi sana vinaweza kuwa sumu kwa mimea. Hii mara nyingi hushuhudiwa na dalili za mmea kuunguzwa na chumvi lakini ukipima udongo wako nitakuambia utumie mbolea gani zaidi na kwa kiasi gani kulingana na ukubwa wa shamba lako na zao unalolima kitaalamu zaidi. Dalili hizi hujumuisha majani kuwa ya kahawia pembezoni, ikitengwa na sehemu za kijani na mduara mdogo wa njano. Mwelekeo huu wa majani kuwa kahawia, ambao ni kuonyesha kifo cha majani, kuanzia kwenye ncha na kuendelea hadi shina la jani kupitia pembezoni mwa jani.
Udongo usio na asidi wala alikali (huru)
KIFAA CHA KUPIMIA UDONGO |
No comments: