HALI YA BIASHARA KWA SASA KATIKA SOKO LA MAWENZI MKOANI MOROGORO.
Mwenyekiti wa soko la Mawenzi mkoani morogoro Ramadhani Mohamedi ametoa
ufafanuzi juu ya hali ya biashara kwa kipindi cha sasa
ambapo kumekuwa na ongezeko kubwa
la bei ya nyanya inayosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha mashambani na kusababisha nyanya nyingi
kuharibika.
Ramadhani Mohamedi amesema
kuwa kuna baadhi ya bidhaa zilizo panda bei ususani zao la nyanya ambalo kwa
kipindi hiki bei yake imekuwa ghali kutokana na nyanya nyingi kuozea shambani
na kushwindwa kustahimili maji mengi yatokanayo na mvua.
Aidha, ameongeza kwa kuwataka wafanya biashara
wanaojishughulisha na uuzwaji wa bidhaa katika soko hilo kufuata taratibu na
kanuni zilizo wekwa katika soko hilo ili kila mmoja aweze kunufaika kwa kufanya
shughuli ya biashara katika hali ya
ufanisi na kushirikiana na viongozi wa
soko hilo.
Halikadhalika
mmoja wa mfanya biashara katika soko hilo
Cosmas Pascal, ameongeza kwa kusema kuwa katika msimu huu nyanya hulazimika kupanda bei kutokana na
nyanya nyingi kuharibika shambani kutokana na wingi wa mvua kunyesha na kupelekea nyanya nyingi kupasuka
na nyingine kuoza hasa zikiwa bado shambani.
Hata hivyo kila mnunuzi wa bidhaa katika soko hilo
anatakiwa kuto mkabidhi mzigo kijana yeyote asiye na vazi rasmi lenye namba ya
utambulisho ili kuepukana na wingi wa matukio ya wizi yatokanayo na vijana
wengi kujihusisha na kubeba mizigo ya mnunuzi na hatimaye kutokomea kusiko
julikana.
No comments: